Friday, August 23, 2013

Amir Shekh Kundecha aliwekwa kizuizini.

Leo katika swala ya ijumaa katika mskiti wa almarhum SHEKH Idrisa
Al akh SHEKH Basaleh akizungumza nawaislamu Mara baada ya swalatul Juma'  alisema juu ya kadhia ya SHEKH Ponda nakwamba serikali haikuwa na ufahamu wakujua wamemkamatia nini SHEKH Ponda.  kwakua wali dhamiria kwanamna yoyote kumnyima haki SHEKH huyo kwa namna yoyote kutokana na ukweli ambao anao uzungumza."kwanini wamfungulie mashtaka haraka nakatika hali ile akiwa hospitali halafu badala yake  wayafute napia siku hiyo hiyo kwa haraka,na tena wakampeleka Morogoro kumfungulia mashtaka mengine ? Hii ni dhahiri kwamba wamedhamiria kupindisha haki kiasi kwamba hawafaamu nini wanacho mshtakia au ni kosagani hasa wampachike" pia katika halinyingine SHEKH Basaleh amezungumza kuwa katika hali isio eleweka SHEKH Kundecha ambaye ni amir wa Taasisi na jumuia za kiislamu hapa nchini aliitwa na police jijini kwa mahojiano kisha wakamuweka kizuizini mpaka pale alipo tolewa kwa dhamana. vilevile mashekh wengine watakiwa kuripoti kituoni akiwemo SHEKH Kondo Bungo,amakwa hakika wamedhamiria kuupiga vita uislamu hapa nchini nasijui baada ya hao nani anafuata, alisema hayo SHEKH Basaleh. Pia SHEKH aliwataka waislamu wawe na mshikamano na umoja pamoja na subira, kwa kua tumeimizwa sana kuwa na subira katika kuyaendea matatizo yetu.Kwakuongezea pia SHEKH amesema inavyoonekana watu hawaujui uislamu ulivyo na kua uislamu ni dini ya kufanya mema na kukatazana mabaya hivyo nijuu ya kila muislamu anapo liona baya alitoe kwa mkono wake ama alikemee hivyo ni juu yetu waislamu kukemea maovu ndani ya nchi hii nakwamba serikali kwa matumizi yake ya mabavu itakwenda kuipeleka nchi hii pabaya kwani viongozi wengi wa kidini na siasa wamelaani juu ya tukio alilo fanyiwa SHEKH Ponda wakiwemo mapadri pia ambao pia wameiambia serikali kua, kwa matumizi yake ya mabavu itaipeleka nchi kubaya.

No comments:

Post a Comment

tafadhali tuandikie maoni yako.