Tuesday, November 19, 2013

Mtazamo kuhusu machafuko huko parestina.

kinacho faamika nawengi kuhusu parestina si uhalisia halisi juu ya swala lenyewe na uhalisia wake na mantiki ya kadhia nzima juu ya mauaji yanayo tokea na swalazima la upoteaji wa haki za kibina damu katika nchi ya kiyahudi au ardhi ya parestina, matukio mengi huusishwa na swalazima la marekani najitihadazao za kuupiga vita huislam duniani kote, ndio kiuhalisia tunaweza sema kua kuna ukweli juu ya hili, lakini swali lakujiuliza ni, myahudi ni nani? nilipi taifa la kiyahudi? na kwanini myahudi achague ardhi ya parestina? kwanini mmarekani amsaidie myahudi? ukiweza jibu maswali hayo fika uta weza kutambua chanzo na sababu zinazo na zilizo pelekea vita migogoro katika Middle East. Kwa mtazamo tu waharaka swala hapa si mtazamo wa kidini kama inavyo zaniwa, nawala si kweli kwamba eti wayahudi wamekalia ardhi ya parestina kwakua tu imeandikwa katika maandiko matakatifu ya kikristo ( Bible ) kuwa wamehaidiwa kuishi hapo la khasha, bali ni swala zima la kimaslahi na unyanyaswaji,tamaa na roho ya kutu itokanayo na Historia chungu waliyo nayo wana wa izrael (wayahudi), hivyo basi kutokana na historia ya unyonywaji na ukandamizwaji iliyo wahi kuwatokea wayahudi ime wapelekea wao kutanga na kuhangaika nakwenda hovyo pasipo kujua. Na hatimaye kutokana na sababu hizohizo za uchu na roho ya kutu ndizo zilizo ipelekea marekani kutaka kuisaidia izrael katika kuwatawala waparestina ambao miongoni mwao ni waislamu. Hivyo basi hifahamike yakwamba ugomvi uliokuapo pale umebezi zaidi katika swala la kimaslahi na wala si lakidini kama inavyo dhaniwa na watu wengi duniani.Umwagajidamu unaoendelea hasa kwa watoto na wakina mama ni dhahiri kwamba, swala hili si lakidini kwani kuna waparestina wakristo naopia wana poteza maishakilasiku kutokana na udhalimu wa Wamarekani na wayahudi. Jamain jamani ! shime kwa watu wooote wapenda amani duniani tukemee na kupinga vitendo hivi vya kidhalilishaji na ukandamizaji vinavyo endelea kufanywa na wayahudi na marekani dhidi ya parestina.naiunga mkono serikali ya Tanzania kwakua haiungi mkono vitendo hivyo na pia chuo kikuu cha kiislamu cha morogoro kwa kuweza kuandaaa kongamano ambalo liliweza kufumbua macho wasomi wengi wa morogoro juu ya swala zima linalo endelea huko Middle East.
Hitimisho utajiri ulipo Middle East ndio ulio waponza waparestina jiulize kwanini myahudi aliondoka Uganda kwanini hakukaa Nigeria au kwengineko? Na nikwanini marekani haingilii migogoro ya nchi kame za kiafrika?  Kwani Somalia imekua katika mgogoro kwa miaka mingapi? Kongo je? Swala hapa ni maslahi kwanza.Mwakim jk nyerere alisha zungumza kwenye hotuba zake "watu Hawa saidii Kongo kuna nini Kongo zaidi yamigomba ya ndizi sasa watu wanatakandizi?.

No comments:

Post a Comment

tafadhali tuandikie maoni yako.