Monday, April 27, 2015

Wakati wa uchaguzi mauaji na ukatili dhidi ya ma Albino huongezeka kwa nini?

Ni dhahiri na utakubaliana nami kwamba tunapofika au pindi tu tunapo karibia na uchaguzi mkuu hapakwetu Tanzania ndipo pia vitendo vya ukatili na mauaji dhidi ya nduguzetu maalbino huwa vinakithiri na kukua kwa kasi katika kipindi au vipindi hivyo. Maswali ya kujiuliza, ni kwanini hali kama hii iwe hivi? Na huu ni utafiti tu mdogo ambao hauitaji huwe na PhD au sampuri yake , hata mlevi ataligundua hilo kwakua jambo lenyewe liwazi sana , sasa basi hawa wachunguzi wa unyama huu wamegundua nini? Wanafanya nini? Nakama mauaji na ukatili dhidi ya albino yanatokana na sababu za watu kujipatia utajiri wako wapi hao watu? Mbona hawakamatwi nabadala yake ni walala hoi tuu ambao ni watu wakawaida tu ndio tunasikia wametiwa mbaroni na kufanyiwa uchunguzi, hao matajiri wako wapi? Nidhahiri kuwa jambo hili pia lina husishwa na nguvu kubwa na nguvu hiyo inatokana na siasa, upoukweli naniukweli usiojificha kuwa wapo baadhi ya viongozi na wanasiasa wanao jihusisha kwanamna moja au nyingine katika ukatili na mauaji dhidi ya ndugu zetu ma albino, nani wazi kwamba hawa watu wanatumia nguvu nyingi kuficha uovu wao huo na ndio maana kasi ya mauaji na ukatili dhidi ya ma albino inakua kwakasi kutolingana na juhudi za jeshi la polisi katika kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo. Hii inaonesha kwamba serikali yetu imefeli katika swala hili kama ilivyo feli katika kupambana na madawa ya kulevya hapa nchini kutokana na kwamba hao wanao kemea na kulaani vitendo hivi vya ukatili na uwaji wa ndugu zetu ma albino ndio haohao wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kinyama. Ifikie mahali watanzania tuwe na uchungu dhidi yetu wenyewe, hawa watu tunawajuwa kwakuwa ni wana jamii kama sisi ila kwasababu zetu wenyewe tunawafumbia macho. Wapo watu wanataka uongozi nahata umaarufu na mafanikio ya kisisa kwa kupitia njia hizi haramu.kama mganga wa kienyeji anapewa kibali na anatambulika kisheria,mauaji yatapungua? Serikali yetu haitambui uchawi inatoa vibali kwa waganga vya nini? Kwa nini ma Albino wana uawa kwa nini wanafanyiwa ukatili…? Ni kwasababu hizi zakishirikina na uchawi ambazo pia zinahusisha viongozi wetu waliopo madarakani. Sasa kwanini serikali isishikilie msimamo wake wakuto aminiuchawi nakutokomeza maswala haya yakishirikina yasiokuwa na tija? Kwanini serikali ina acha maswala haya ya uganga kufanywa waziwazi wakati tatizo tulilo nalo juu ya wenzetu ma albino linahusiana mojakwa moja na maswala haya? Huu uchunguzi unafanywa mpakalini wakati nduguzetu wanapotea? Ipo haja ya kukemea na kuonesha juhudi ya kufuatilia kwa ukaribu juu ya mambo kama haya, pamoja na kuonesha ushirikiano katika kuhakikisha tunafanya juhudi za kutokomeza ukatili huu si vyombo vya sheria tu peke yake bali niswala letu wote kama wana jamii.
image

No comments:

Post a Comment

tafadhali tuandikie maoni yako.